February 9 2016 waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi Mwigulu Nchemba alilazimika kusafiri haraka hadi mkoani Morogoro kijiji cha Kambala wilaya ya Mvomero,
baada ya taarifa za mapigano ya wakulima na wafugaji kumfikia, safari
hii yameingia kwenye headlines nyingine ya kuuwawa zaidi ya mifugo 75
kati ya mifugo 200 waliojeruhiwa kwa mapanga.
Waziri Mwigulu
amefika eneo la tukio na kuchukua hatua za haraka kwa kuagiza kamati ya
ulinzi ya mkoa na wilaya, kufanya uchunguzi na kuwatafuta wahusika wa
tukio la kukatwa katwa mapanga kwa zaidi ya mifugo 75, ili wafike mbele
ya mikono ya sheria nakuagiza mahakama kupitia upya hukumu
iliyotolewa mwaka 2015 ya kugawa mipaka kati ya eneo la wakulima na
wafugaji.
Mwisho waziri Nchemba
ameagiza uongozi wa mkoa na wilaya kufanya mkutano wa hadhara wa
wakulima na wafugaji tarehe 20/02/2016, ili kuanza harakati za kumaliza
mgogoro. Kati ya mifugo inayotajwa ni mbuzi, kondoo na ndama.
0 comments:
Post a Comment