Katika kuhakikisha wananchi wa Jimbo la
Ilemela wananufaika na huduma bora za afya
Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Naibu Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula amewachangia
wananchi waliokuwa tayari kunufaika na huduma ya mfuko wa afya wa Tiba kwa Kadi
(TIKA) itakayowawezesha kupata huduma bure za afya kwa kutumia kadi
inayopatikana kwa kuchangia elfu Ishirini kwa Mwaka.
Zoezi hilo limefanyika Kata ya Sangabuye Jimboni
humo alipokuwa akikabidhi gari la kubebea wagonjwa lililotolewa na Wizara ya
Afya kupitia Benki ya Dunia ikishirikiana na Mfuko wa fedha duniani hivi
karibuni na kuwataka wananchi kulitunza huku akiwaasa watumishi kulitumia gari
hilo kwa Kazi iliyokusudiwa.
Akizungumza na wanachi hao Dkt Mabula amesema.
'...Niwaombe mlitunze gari hili na mlitumie kwa
kazi iliyokusudiwa kituo hiki cha afya kinaangaliwa kwa jicho la ziada
kulingana na eneo linalohudumia kuwa kubwa sana hivyo kila mmoja
anapaswa kuwa mlinzi wa rasilimali zetu na msiache mkazani mnaikomoa Serikali
au Mnamkomoa Mbunge hizi ni Mali zenu...'
Aidha Mhe Dkt Mabula amewaasa wananchi kuacha
kununua dawa kiholela bila ushauri wa daktari sambamba na kushirikiana
ktk kujenga Nyumba za watumishi mbalimbali wakiwemo wahudumu wa afya.
Wakati huo huo Dkt Mabula ametembelea
miradi ya madaraja inayoendelea Jimboni humo, Shule ya Sekondari
Sangabuye, Shule ya Msingi Bugogwa, Kisundi na Igombe lengo likiwa ni
kusikiliza Kero zinazowakabili na kuzipatia ufumbuzi sanjari na kufatilia Zoezi
la Uandikishaji wanafunzi linaloendelea mashuleni.
Nao wananchi waliohudhuria makabidhiano hayo
wakiongozwa na Diwani wao ambae pia ndio Meya wa Manispaa Ilemela Mhe Renatus
Mulunga wamemshukuru Mbunge huyo kwa Jitihada anazozifanya katika kuhakikisha
anawaletea maendeleo na kumhakikishia
ushirikiano wa dhati ili kujiletea maendeleo kwa Umoja.
ushirikiano wa dhati ili kujiletea maendeleo kwa Umoja.
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
Hakika tuko pamoja ktk maendeleo ya jimbo letu la ilemela pamoja tushirikiane kuijenga ilemela,,,ilemela ni yetu kila mmja ana jukum la kumsaport hon mbunge ktk kutatua matatizoo,,,ya wana ilemela naunga mkono jitihada anazozifanya
ReplyDelete