Mbunge wa jimbo la Ilemela Mh.Dkt.Angeline.S.L.Mabula, amewapongeza
wanafunzi,walimu,wasimamizi wa idara ya Elimu na wadau wa Elimu katika jimbo la
Ilemela kwa matokeo mazuri ya kidato cha nne.
Katika matokeo ya mwaka huu,Manispaa ya Ilemela imeshika nafasi
ya sita katika manispaa 10 bora nchini katika matokeo ya mwaka huu.
Mh.Mbunge anaamini kuwa matokeo haya ni juhudi zilizo fanywa
vyema na kila mtu ndani ya jimbo letu kwa kutimiza wajibu wake ili kufikia
hatua hii.
Mh.mbunge amesisitiza kutimiza ahadi yake yakutoa zawadi kwa
shule zilizo fanya vizuri,na kuwatia moyo na kuzijengea uwezo shule ambazo
hazijafanya vizuri.
"Ilemela ni yetu,tushirikiane
kuijenga".
Imetolewa
na.
Ofisi
ya mbunge.
Jimbo
la Ilemela.
31/Jan/2017
0 comments:
Post a Comment