Baada ya kuwepa
kwa ugomvi wa kungombea mpaka kati ya
wananchi wa kijiji cha Irole wilaya ya Kilolo
na Ilambilole katika wilaya ya Iringa ,naibu waziri wa
ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Dkt. Angeline Mabula
amepiga marufuku wananchi kutumia eneo linalogombewa
hadi hapo wizara yake itakapotuma wataalam kwa ajili ya
kubainisha mpaka utakaotenganisha wilaya ya Kilolo na Iringa.
Mbali ya kuzuia
wananchi kutumia eneo hilo la Irole pia naibu
waziri huyo amemzuia mmoja kati ya wafugaji wa
jamii ya kimasai kuendelea na ujenzi wa nyumba
katika eneo hilo na kuliagiza jeshi
la polisi wilaya ya Iringa na Kilolo kuchukua hatua kali kwa
yeyote atakayepuuza agizo hilo.
Awaagiza wakuu wa wilaya
ya Iringa Richard Kasesela na mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia
Abdalah kuitisha mkutano wa pamoja kati ya wananchi wa
Ilambilole wilaya ya Iringa na Irole wilaya ya Kilolo
ili kuona jinsi gani wanavyoishi wananchi
wa pande hizo mbili na sio kuweka mipaka upya.
Akito agizo hilo jana
wakati wa mkutano wake na wananchi wa Irole
na viongozi kutoka wilaya ya Iringa na Kilolo
naibu waziri huyo alisema kuwa akiwa
naibu waziri kutoka wizara yenye dhamana
na mipaka ya nchi hii yote kuwa zoezi la utambuzi
wa mipaka hiyo litafanyika ndani ya
mwezi huu na kwa sasa ni marufuku kwa
mtu yeyote kuendelea na shughuli yeyote iwe ya
ufugaji ,kilimo ama ujenzi katika eneo hilo la Irole hadi
wataalam watakapofika kubainisha mipaka kati ya
wilaya ya Kilolo na Iringa na baada ya hapo itatambuliwa
mipaka kati ya kijiji na kijiji kama njia ya
kumaliza tofauti zilizopo kwa wananchi hao .
Alisema kuwa mpaka
wowote lazima useme ni gazeti gani la
serikali lilitangaza katika mipaka ya Kilolo na Iringa
ambayo ilizaa Kilolo waliweka GN yao namba 366
ya mwaka 2002 hivyo mipaka hiyo
ndio inayotambuliwa na si vinginevyo .
" Iwapo kama mpaka
wa wilaya na wilaya hauna tatizo iweje kuwe na
mgogoro wa mipaka ya kijiji wakati mipaka ya wilaya
ipo sawa ......naomba kusema kuwa mwananchi
wa Kilolo kulima eneo la Iringa ama mwananchi wa Iringa
kulima ama kufanya shughuli zake katika wilaya ya
kilolo si tatizo na huwezi sema ni mgogoro mtu anaweza
kulima ama kufanya shughuli zake popote pale bora mradi
asivunje sheria"
Hivyo alisema kila
mwananchi anaweza kumiliki ardhi popote pale ila
sio kubadili mipaka ili kulifanya eneo lake kuwa
wilaya anayoitaka yeye kwa hiyo katika
hili ifahamike kuwa gazeti la serikali la 366 la mwaka
2002 linalobainisha mipaka ndilo litakalotumika kuamua
na kuonyesha mipaka hiyo na kuwa hakuna sababu ya
wananchi kuendelea kugombana kwa ajili ya ardhi kwani kila aliye na
ardhi yake iwe Iringa ama Kilolo ataendelea kumiliki yeye
mwenyewe .
Awali mbunge wa
Kilolo Venance Mwamoto alimweleza naibu
waziri huyo kuwa kimsingi wananchi wa Irole wilaya
ya Kilolo ndio ambao wanauhitaji wa eneo hilo na
ndio sababu wamefika katika mkutano huo ila wananchi wa
Ilambilole hawana uhitaji wa eneo hilo zaidi ya mfugaji mmoja
aliyepo eneo hilo la mpaka anayeingiza mifugo katika mashamba
ya wakulima .
Alisema kuwa siku
zote mgogoro huo ni wa pande mbili ila katika
hilo inaonyesha wananchi wa Ilambilole hawana shida na
eneo hilo isipo kuwa kuna mtu mmoja anayekuza jambo hilo kwa kutaka
kwa manufaa yake na kutokana na ukweli huo ni vema serikali
kuangalia namna gani ya kuwaachia wananchi wa Irole eneo hilo .
0 comments:
Post a Comment