Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameendelea na Ziara yake ya kusikiliza kero za Ardhi na kutatua changamoto mbalimbali za Ardhi kwa wananchi.
Ziara hiyo iliyojumuisha Mikoa ya Ruvuma, Iringa, Njombe, Katavi, Mbeya, Songwe na Leo imeendelea Mkoani Mtwara.
Ziara imehusisha upokeaji wa taarifa za wilaya na Mikoa, Mazungumzo na Mabaraza ya Ardhi, Kuzungumza na Wananchi kupitia Mikutano ya Hadhara, Kuzungumza na Watumishi, Kukabidhi Hati, Mazoezi ya Urasimishaji Makazi, Kukagua Mifumo ya Ulipaji wa Kodi za Ardhi, na Ukaguzi wa Miradi Mbalimbali ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Akizungumza katika moja ya mikutano yake ya hadhara Mhe Naibu Waziri Mabula amewataka Wananchi kutunza mazingira yanayowazunguka kwa kuwa na matumizi bora na sahihi ya Ardhi huku akiwaasa juu ya umuhimu wa zoezi la urasimishaji makazi.
'... Niwaombe mtunze Mazingira kwa kufuata matumizi sahihi ya Ardhi...' Alisisitiza
'...Ilemela ni yetu,Tushirikiane kuijenga...'
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
17.01.2017
0 comments:
Post a Comment