Mbunge wa Jimbo la Ilemela-Mwanza,na Naibu Waziri Wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Nchini Dkt.Angeline Mabula hii Leo amejumuika na wadau wa maendeleo mbali mbali duniani Katika warsha ya *"2016 Global SAEMAUL UNDONG forum"* Unaoendelea Korea Kusini.
katika warsha ambayo Mataifa mbali mbali zaidi ya 50 duniani yatajadili mkakati wa maendeleo endelevu.
Pamoja na warsha hiyo Mh Mbunge amefanya vikao mbalimbali hapa nchini korea Kusini na wakuu wa mashirika na makampuni mbalimbali ilikuona ni namna gani wanaweza kusaidia katika kuharakisha Maendeleo ya Jimbo letu.
Mh Mbunge wa jimbo la Ilemela Dkt.Angeline Mabula atakuwa nchini korea ya Kusini kwa muda wa siku tatu nakisha kurejea jimboni kwa ajili ya harambee kubwa ya Mfuko wa Elimu itakayofanyika tar 9 July 2016 Itakayo hudhuriwa na Mh.Waziri mkuu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh Kassim Majaliwa Kassimu.
"ilemela ni yetu,tushirikiane kuijenga".
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge.
Jimbo LA Ilemela-Mwanza.
0 comments:
Post a Comment