Ikiwa ni siku ya pili Katika
Mkutano wa *"2016 Global SAEMAUL NDONG Forum "* Unaoendelea hapa nchini
Korea kusini. Mh.mbunge wa jimbo la Ilemela -Mwanza na Naibu Waziri wa
aridhi nyumba na maendeleo ya makazi Dkt.Angeline Mabula amewataka
vijana wakitanzania wanao Soma katika Mataifa mbalimbali Duniani kurudi
nyumbani Mara baada ya Kuhitimu masomo yao ili kutumia Elimu,Ujuzi na
Uzoefu wa mambo Mbali mbali wayapatayo katika Mataifa hayo Kwa Kuwa
Wazalendo Kwa kuja kuitumikia na kusaidia kuliendeleza Taifa letu.
Mh.mbunge wa jimbo la Ilemela -Mwanza na Naibu Waziri wa aridhi nyumba
na maendeleo ya makazi Dkt.Angeline Mabula ameyasema hayo wakati
akiwasilisha Mada ya hali ya Ongezeko la watu na maendeleo nchini
Tanzania. katika hatua nyingine Mh Dkt Angeline Mabula ameendelea
kuwasihi Wadau Mbali mbali wa Maendeleo kuitumia fursa ilio tolewa na
Tanzania ya kuimarisha Ujenzi wa Viwanda kuja kuwekeza kwa wingi na
hatimae kuchochea maendeleo ya watu wa Afrika kwa kuwaongezea
kipato,Ajira na uhakika wa huduma za msingi katika jamii
Mkutano huu utakamilika kesho na kuhitimishwa na Mataifa mbalimbali kwa kutoa Dira ya maendeleo katika maeneo yao.
"Ilemela ni yetu,tushirikiane kuijenga"
Imetolewa na ofisi ya Mbunge
Jimbo la ilemela-Mwanza
0 comments:
Post a Comment