Katika Hali ya kuendelea kupanua wigo wa mahusino bora kwa manufaa ya watu wetu,Mh.mbunge wa jimbo la Ilemela-mwanza na Naibu waziri wa Aridhi nyumba na maendeleo ya makazi nchini Dkt Angeline Mabula amefungua ukurasa wa mahusiano ya ushirikiano baina ya manispaa ya Ilemela na mji wa Daegu nchini korea kusini.mh mbunge amekutana na kufanya mazungumzo na meya wa mji wa Daegu na kukubaliana kishirikiana na manispaa yetu kama mji Dada.kuanzishwa kwa mahusiano haya kutaisaidia wilaya ya Ilemela kutatua kero ya maji,elimu na mafunzo kwa vijana,fursa ya kubadilishana tamaduni na uboreshaji wa Huduma na utendaji wa miji yetu.mheshimiwa mbunge ana amini mahusiano haya mapya ya miji yetu hii miwili ya Daegu na Ilemela yatafungua fursa pana kwa manispaa yetu na watu wake.Mh.mbunge yuko nchini Korea kwa mwaliko maalumu wa mkutano wa semaul dong nchini Korea kusini."Ilemela ni yetu,tushirikiane kuijenga".
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge.
Jimbo LA
ilemela-Mwanza
0 comments:
Post a Comment