Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ndugu John Mongela amewaapisha rasmi
wakuu wa wilaya wa teule wa wilaya saba za mkoa wa mwanza .zoezi hilo
limefanyika ktk viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa na kuhudhuriwa na viongozi
mbalimbali wa dini,chama na serikali. Akizumgumza na Waandishi wa habari baada
ya zoezi hilo,Mbunge wa jimbo la ilemela na naibu waziri wa aridhi nyumba na
maendeleo ya makazi Dkt.Angeline Mabula amewapongeza wateule wote na kwa niaba
ya wabunge wa majimbo yote ya Mwanza amewasii na kuwaelezea ya kuwa
"nimewahi pia kuwa mkuu wa wilaya kabla ya kuwa mbunge na naibu
waziri,hivyo nafahamu vyema dhima na majukumu ya nafasi ya mkuu wa Wilaya
nnawaahidi Ushirikiano na kuwaomba kuwa chachu ya kusaidia kuwapunguzia na kuwaondolea
wananchi tabu,kero,na matatizo mbalimbali katika wilaya zote. "Ilemela ni
yetu,tushirikiane kuijenga".
Imetolewa na
Ofisi ya mbunge.
Jimbo la ilemela-mwanza.
0 comments:
Post a Comment