MKURUGENZI WA MANISPAA UBUNGO AZURU OFISI YA MBUNGE ILEMELA.
Mkurugenzi wa
Manispaa ya Ubungo Comred John Kayombo Leo mapema amezuru Ofisi ya Mbunge wa
Jimbo la Ilemela-Mwanza na kutoa Pongezi za Dhati kwa Juhudi zinazofanywa na
Mbunge wa Jimbo hilo Mhe .Dkt Angelina Mabula ktk kuwa wakilisha na kuwatumikia
wananchi wa Jimbo hilo,
Pia Mhe. Kayombo
ametumia fursa hiyo kutoa heko kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilemela,Mbunge na viongozi
wa chama kwa namna walivyo umaliza mgogoro wa wafanya biashara wa soko la
Kirumba kwa hekima na mafanikio makubwa kwa maslahi ya wananchi wanyonge.
Comred Kayombo ni
miongoni mwa wadau na washauri wakaribu wa maendeleo ya Jimbo la Ilemela.
"Ilemela ni yetu, Tushirikiane kuijenga"
Imetolewa na Ofisi ya Mbunge.
Jimbo LA ilemela-Mwanza.
0 comments:
Post a Comment