Katika hali ya kuanza kutimia kwa ndoto ya
kuuinua na kuimarisha uchumi wa wananchi wa Jimbo la Ilemela kwa njia ya
Uwekezaji mkubwa, Mhe Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dkt. Angeline S.L. Mabula
amepokea ujumbe wa wawekezaji 19 kutoka nchini korea kusini hii leo kwa lengo
la kufungua rasmi shughuli za uwekezaji mkubwa Jimboni hapa.
Wawekezaji hao wamefanya mazungumzo rasmi na Mhe
Mbunge na kuahidi kutumia fursa ya uwekezaji walioipata, kuzalisha ajira,
kukuza uzalishaji, kuchangia pato la taifa, na kusaidia kutoa huduma mbalimbali
za jamii.
Ugeni huu ni matunda ya ziara ya Mhe Mbunge wetu
aliyoifanya nchini Korea Kusini mapema mwaka huu.
"ilemela
ni yetu,tushirikiane kuijenga"
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
Septemba 21,2016
0 comments:
Post a Comment