Ugeni wa wawekezaji wa maeneo mbalimbali ya
kiuchumi umewasili rasmi wilaya ya Ilemela ukihusisha wawekezaji wa Maji na
Kilimo, Ujenzi, Michezo, Usafi wa Miji, Mafunzo na Ufundi, Viawanda vya Nguo,
Habari na Mawasiliano, Ugeni huo umefanya ziara katika maeneo mbalimbali ya
uwekezaji yanayopatikana Wilaya ya Ilemela yakiwemo Chuo cha Ufundi VETA, Idara
ya Maji MWAUWASA, na Kiwanda cha Nguo MWATEX.
Akizungumza katika ziara hiyo mwenyeji wa Ugeni
huo Mhe Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo
ya Makazi Dkt. Angeline Mabula amesema kuwa ujio wa Ugeni huo unatokana na
ziara yake aliyoifanya nchini Korea mapema mwaka huu lengo likiwa ni
kukaribisha uwekezaji mkubwa ili kuboresha huduma za kijamii, kukuza uchumi,
kutengeneza ajira na kuimarisha mahusiano ya nchi yetu na nchi ya korea katika
duru za kiuchumi.
Nae kiongozi mkuu wa Wawekezaji hao Ndugu Park In
Hwan amesema kuwa amefurahishwa na ushirikiano mzuri wanaoupata kutoka Tanzania
huku akiipongeza serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt.
Magufuli iliyojidhatiti katika kupunguza umasikini na kupambana na rushwa
kunakoambatana na lengo lao la uwekezaji ili kutoa Ajira , Kupunguza Umasikini
na kuliletea Taifa Maendeleo.
Ugeni huo pia unataraji kukutana na
Uongozi wa Halmashauri ya Manispaa Ilemela na Mkoa Mwanza siku ya
Jumatatu Tarehe 26.09.2016 ili kujadili mambo mbalimbali ikiwemo fursa za uwekezaji
zinazopatika mkoani humo.
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge Ilemela
25.09.2016
0 comments:
Post a Comment