Msafara wa wawekezaji na wataalamu 19 Kutoka
Nchini Korea Kusini walio wasili wilayani Ilemela kwa Mwaliko wa Mbunge
wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt
Angeline.S.L Mabula wazaa matunda.
Wageni hao ambao walipata fursa ya kuzungumza na
Uongozi wa Mkoa chini ya Mhe Mkuu wa Mkoa Comred John Mongela pamoja na Uongozi
wa Halimashauri ya Manispaa ya Ilemela umeamua kimsingi kujenga kiwanda kikubwa
cha nguo wilayani Ilemela, kuanzisha kiwanda cha uzalishaji wa umeme kwa nguvu
ya jua, kuanzisha radio ya watu wa Ilemela, kuboresha chuo cha ufundi cha veta
na kukiwezesha kwa kukipa vifaa vikubwa vya kisasa, kuanzisha kituo kikubwa cha
mchezo wa soka ili kuwajengea uwezo wachezaji wetu wa Ilemela kupata soko la
kucheza ktk timu za kimataifa zikiwemo timu za Korea kusini.
Lakini pia wataisaidia Mamlaka ya Maji Mwanza kuboresha Miundo mbinu ya Maji ili Wananchi wengi wapate Maji tofauti na hali ilivyo sasa
Mazungumzo hayo yalifatiwa na Zoezi muhimu la
kusaini hati za Makubaliano (MOU) ili mchakato wa mambo yote uweze kuanza.
Wageni wetu hawa
walikamilisha ratiba yao hapa nchini kwa kukutana na kufanya mazungumzo na Mhe
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa ambae
Amempongeza Mhe Mbunge kwa juhudi zake na kuwaahidi ushirikiano wageni
wetu kwa niaba ya
serikali.
"Ilemela ni yetu,tushirikiane kuijenga". Imetolewa na
Ofisi ya mbunge
Jimbo la Ilemela~Mwanza
0 comments:
Post a Comment