Juhudi za Mbunge
wa Jimbo la Ilemela Dkt. Angeline.S.L.Mabula ktk Harakati za Kuwawakilisha,
Kuwatumikia na Kusukuma kasi ya Maendeleo ya Wananchi Wenzake wa Jimbo la
Ilemela ktk nyanja ya Elimu, Afya, Miundombinu na Huduma za Kijamii, Zimeanza
Kuungwa mkono kwa kasi na Wadau mbalimbali wa maendeleo wenye nia njema na watu
wa Ilemela.
Katika Kuunga
Mkono Juhudi hizo Taasisi ya Mwanza Cosmopoltan Imemkabidhi Mhe. Mbunge
Mifuko704 ya Simenti ili kuunga mkono Juhudi za Mbunge za kuondoa tatizo la
upungufu wa madarasa ktk jimbo letu.
Wakati huohuo Mhe.
mbunge amepokea mchango wa Madawati 30 yenye thamani Shilingi Milioni Tatu
kutoka ktk Taasisi ya umoja wa waendesha bodaboda Wilaya ya Ilemela ikiwa ni
mchango wao wa kuunga mkono juhudi za Mbunge wetu, akiwa ktk zoezi hilo Mhe.
Mbunge pia alipokea mchango wa mfanyabiashara maarufu mkoani Mwanza Ndugu Shah
ambae alifurahishwa na kasi ya utendaji ya Mhe. Mbunge na hivyo kajitolea
kujenga Darasa moja ktk shule ya msingi Tumaini ilioko kata ya Kirumba.
Mhe. Mbunge wetu
amewashukuru watu wote kwa michango yao mbalimbali na kwa ushirikiano wanaompa
ktk kutimiza majukumu ya kuwatumikia wana Ilemela.
"Ilemela
niyetu, tushirikiane
kuijenga"
Imetolewa na
Ofisi ya mbunge
Jimbo la ilemela
Ofisi ya mbunge
Jimbo la ilemela
0 comments:
Post a Comment