Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi
ameipongeza na kuisifu Manispaa ya Ilemela kwa Kasi yake ya Maendeleo sambamba
na Utaratibu wake wa kutatua Migogoro ya Ardhi kwa wananchi.
Hayo ameyasema wakati wa Ziara yake ya kikazi ndani ya Manispaa
hiyo iliyohusisha Ukaguzi wa mifumo inayotumika kulipia kodi ya ardhi, Kikao
cha ndani kilichojumuisha madiwani, viongozi wa wilaya, mkoa na wataalamu wa
ngazi zote na baadae kufanya Mkutano wa hadhara kata ya Mecco unapofanyika
Mradi wa Urasimishaji makazi na kuzungumza na Wananchi wa eneo hilo na
maeneo jirani waliojitokeza kumsikiliza.
‘… Hakuna manispaa yeyote yenye uwezo wa kuendelea kwa haraka na
muda mfupi kama nyinyi, Nilikuja hapa mara ya mwisho ni tofauti na
nilivyowakuta leo nilikuwa nawaza kuwanunulia mashine za RTK nchi nzima
lakini nyinyi mmeweza kununua wenyewe maanake mmekuwa juu ya wazo langu
na juzi marafiki zenu wa Korea nmesaini barua wanakuja na mfumo wa uboreshaji
na usimamizi wa ardhi …’ Alisema.
Aidha Mhe Lukuvi ameongeza kuwa ipo haja ya kufundisha manispaa
nyengine utataribu unaotumika katika kutatua migogoro ya ardhi nakuahidi kuwa
yupo teyari kusaidia mawasiliano na wizara nyengine unapotokea uhitaji kwa
migogoro itakayohusisha taasisi zaidi ya moja huku akitaka kutafuta namna
nyengine ya kuhakikisha juhudi katika ukusanyaji wa kodi za ardhi na utoaji
wa hati zinaongezeka ili kuiongezea nchi pato litalosaidia utekelezaji wa
miradi mbalimbali ya maendeleo.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa Mwanza Mhe John Mongela mbali na
kumshukuru kwa kuutembelea mkoa wake mara kwa mara hasa Ilemela ameahidi kuiga
mfano wake kwa kurudi Ilemela kutatua changamoto za ardhi zitazoshindikana kwa
ngazi ya wilaya.
Wakihitimisha kwa wazo la pamoja mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe
Dkt Leonard Masale, Meya wa manispaa hiyo Mhe Renatus Mulunga na Mkurugenzi
wake Ndugu John Wanga wamemuhakikishia kuwa watatekeleza maelekezo yote
aliyoyatoa katika ziara yake haraka iwezekanavyo sambamba na kumpongeza Naibu
Waziri wa Ardhi na Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dkt Angeline Mabula katika
kusaidia utatuzi wa changamoto za ardhi na utekelezaji wa shughuli za maendeleo.
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
29.04.2017
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
29.04.2017
0 comments:
Post a Comment