Mbunge
wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt
Angeline Mabula ashiriki maombezi ya kuliombea Taifa na Viongozi wake wote
katika Serikali ya awamu ya Tano chini ya Mhe Rais Dkt John Magufuli
yaliyofanyika katika Viwanja vya Ccm Kirumba na kuhudhuriwa na Viongozi
mbalimbali.
Aidha
katika kongamano hilo lililoandaliwa na akina mama wa kanisa la AICT Dayosisi
ya Mwanza lilidumu kwa muda wa siku tatu ambapo mbali na kuombea Taifa
limezungumzia changamoto mbalimbali anazokumbana nazo Mwanamke,
Mmomonyoko wa maadili kwa Vijana, Namna ya kumkomboa Mwanamke
kiuchumi, Tatizo la Ajira kwa Vijana, na Nafasi ya Mwanamke katika
kulisaidia Taifa.
Akizungumza
katika kongamano hilo Dkt Mabula amewataka Wanawake wote nchini kujisimamia
katika kulisaidia taifa sambamba na kuacha utegemezi kwa kuthubutu na kuchukua
hatua katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Kwa
upande wao wanawake walioshiriki kongamano hilo mbali nakumshukuru Mhe Dkt
Mabula kwa kukubali mwaliko wao wa kuwa Mgeni rasmi katika kuhitimisha kilele
cha kongamano hilo wamemhakikishia kuwa Wanawake wataendelea kuwa msingi imara
katika kuliletea Taifa maendeleo hasa kipindi hiki cha kuelekea Tanzania ya
Viwanda huku Mwanamke akitegemewa kama nyenzo muhimu na chachu ya kuyafikia
malengo hayo kwa kujituma na kuacha utegemezi na mwisho kumkabidhi zawadi ya
picha kwa niaba ya Mhe Janeth Magufuli mke wa Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania kama ishara ya kuthamini na kuutambua mchango wake kama mwanamke
katika kulitumikia Taifa na Msaidizi mahiri wa Mhe Rais.
'
Ilemela ni yetu, Tushirikiane kuijenga'
Imetolewa
naOfisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
0 comments:
Post a Comment