Mbunge WA Jimbo LA
ilemela na naibu waziri Wa Aridhi nyumba na maendeleo ya makazi Dkt.Angeline
Mabula,Leo amezindua harakati za mchezo WA bascket ball kwa wanafunzi WA shule
za msingi na sekondari jimboni ilemela,Akizungumza na wadau WA Michezo pamoja
na wachezaji na viongozi ktk tukio hilo muhimu lililo fanyika ktk uwanja WA kiloleli
wilayani hapa,mheshimiwa Mbunge ameitaka jamii ya wana ilemela kuwekeza ktk
elimu na vipaji vya kimichezo walivyo nao watoto wao ili kujenga Afya zao,
mahusiano,nakujiimarisha kiuchumi kwa kuwa Michezo ni Afya na ni
ajira.mh.Angeline Mabula ni mchezaji mzuri WA bascket ball na amewahi kuwa
kiongozi WA chama cha mchezo huo mkoani Mwanza.Mheshimiwa Mbunge yuko jimboni
anaendelea na shughuli mbalimbali za kuwatumikia wananchi wenzake kabla
hajarejea Dar es laam ktk majukumu ya kitaifa.
Imetolewa
na
Ofisi ya
mbunge.
Jimbo la
ilemela-mwanza.
0 comments:
Post a Comment