Mbunge WA Jimbo LA ilemela na naibu
waziri Wa Aridhi nyumba na maendeleo ya makazi Dkt.Angeline Mabula
(katikati), amefanya ziara ya kukagua Ukarabati wa Miundombinu ya
barabara, mitaro na madaraja katika Kata ya Kirumba Jimboni humo ikiwa ni mwanzo
wa ziara zake katika Kata zote za Manispaa ya Ilemela ili kujionea namna
ukarabati wa mbiundombinu ya barabara unavyoendelea.
Kulia ni Mhandisi wa Manispaa ya
Ilemela, Mikidadi Adam, akitoa taarifa ya ukarabati wa miundombinu katika Kata
ya Kirumba ambapo alibainisha kwamba zaidi ya Shilingi Milioni 195 zimetengwa
kwa ajili ya Kata hiyo ili kukarabati barabara zake ambazo ziliharibika
kutokana na mvua ambapo miongoni mwa barabara zinazokarabatiwa katika Kata
ya Kirumba ni barabara ya Villa, Kabuhoro, CWT-Sabatho.
Mbunge
WA Jimbo LA ilemela na naibu waziri Wa Aridhi nyumba na maendeleo ya makazi
Dkt.Angeline Mabula (wa nne kulia), akiwa katika ziara ya kukagua ukarabati wa
mbiundo mbinu katika Kata ya Kirumba Jimboni humo.
Mitaro
katika barabara ya Villa inaendelea kukarabatiwa ili kuondoa adha ambayo huwa
inajitokeza wakati wa mvua na kusababisha adha kubwa kwa wananchi.
Hii ni barabara ya CWT-Sabatho, awali ilikuwa haitamaniki
kwani ilikuwa ni mashimo tupu. Lakini sasa inapitika vyema na kilichosalia ni
ukarabati wa mitaro ili mvua ikinyesha isiweze kusababisha uharibifu wa
ukarabati huu.
Mbunge
WA Jimbo LA ilemela na naibu waziri Wa Aridhi nyumba na maendeleo ya makazi
Dkt.Angeline Mabula (wa tatu kulia), akiwa katika ziara ya kukagua ukarabati wa
mbiundo mbinu katika Kata ya Kirumba Jimboni humo.
Namna
miundombinu ya barabara na mitaro inavyoendelea kukarabatiwa katika Kata ya
Kirumba, Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza.
Ukaguzi wa miundombinu ya barabara
na mitaro inavyoendelea kukarabatiwa katika Kata ya Kirumba, Manispaa ya
Ilemela mkoani Mwanza.
Pia kuna ujenzi wa daraja katika
barabara ya Kabuhoro Ziwani ambapo kulikuwa na adha kubwa kwa wananchi ambapo
ukarabati huu unaleta ahueni kwa wakazi wa eneo hio pamoja na watumiaji wengine
wa barabara.
Aliagiza ukarabati wa mbiundombinu
ya barabara kukamilika haraka kabla msimu wa mvua haujaanza na kwamba Manispaa
ya Ilemela imetenga Shilingi Milioni 625 ikiwa ni fedha za mfuko wa dharura na
shilingi Milioni 146 ambazo ni fedha za mfuko wa barabara, fedha zote ikiwa ni
kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya barabara.
Mbunge
WA Jimbo LA ilemela na naibu waziri Wa Aridhi nyumba na maendeleo ya makazi
Dkt.Angeline Mabula (mwenye miwani) akiteta kidogo na wakazi wa Kata ya Kirumba
alipotembelea Kata hiyo ili kujionea ukarabati wa miundombinu ya barabara
katika Kata hiyo.
Katibu
wa Mbunge, Kheri James (mwenye kofia) ambapo alisema ofisi ya mbunge
itahakikisha ahadi zilizotolewa na mbunge wakati wa kampeni zinatekelezwa
ikiwemo suala la upatikanaji wa maji na ukarabati wa miundombinu.
Mhandisi
wa Manispaa ya Ilemela, Mikidadi Adam, akitoa taarifa ya ukarabati wa
miundombinu katika Kata ya Kirumba ambapo alibainisha kwamba zaidi ya Shilingi
Milioni 195 zimetengwa kwa ajili ya Kata hiyo ili kukarabati barabara zake
ambazo ziliharibika kutokana na mvua
Diwani wa Kata ya Kirumba, Alex
Ngusa, ambapo alibainisha kwamba barabara za Kata hiyo zilikuwa zimeharibika
sana kutokana na mvua zilizonyesha mwishoni mwanza mwaka jana.
Alishukuru ushirikiano baina yake na
wananchi wa Kata yake, ofisi ya mbunge pamoja na halmashauri ya Manispaa ya
Ilemela na kwamba juhudi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano katika
kuwafikishia wananchi maendeleo zimepokelewa vyema na wananchi huku akiwasihi
kuitunza vyema miundombinu hiyo.
Mmoja wa wakazi wa Kirumba akieleza adha waliyokuwa
wakiipata wakazi wa Kata hiyo kabla ukarabati haujafanyika ambapo aliongeza
kwamba ni vyema ukarabati huo ukaendelea kufanyika hususani katika ujenzi wa
mitaro ili kuondoa adha ambayo huwa inajitokeza wakati wa mvua ikwemo kuharibu
miundombinu ya barabara kutokana na kukosekana kwa mitaro.
Mkazi
wa Kirumba akitoa shukurani zake kwa ukarabati unaofanyika katika barabara za
Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza.
Halmashauri
ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, imeanza ukarabati wa miundombinu ya
barabara kwa kiwango cha changarawe pamoja na mikakati ya ujenzi wa baadhi ya
barabara kwa kiwango cha lami.
Akikagua
zoezi la ukarabati wa miundombinu ya barabara katika Kata ya kirumba, Mbunge wa
Jimbo la Ilemela, Angelina Mabula, ametaka ukarabati wa miundombinu hiyo
ikiwemo mitaro, kukamilika mapema kabla msimu wa mvua haujaanza ili kuepukana
na athari za mvua.
Amesema
katika kipindi cha miaka mitano, hali ya miundo mbinu ya barabara katika jimbo
hilo itakuwa katika hali nzuri na hivyo kupunguza kero ya ubovu wa miundombinu
ambayo imekuwepo kwa muda mrefu katika Manispaa ya Ilemela.
Mhandisi
wa Manispaa ya Ilemela, Mikidadi Adam, amesema Manispaa hiyo imetenga shilingi
Milioni 625 zilizotokana na fedha za mfuko wa dharura na barabara kwa ajili ya
ukarabati wa miundombinu ya barabara katika manispaa hiyo japo amebainisha
kwamba bado fedha hizo hazitoshi hivyo ni vyema serikali ikaendelea kutenga
fedha zaidi kwa ajili ya kutekeleza ukarabari huo.
Wakati
ukarabati huo ukiendelea, diwani wa Kata ya Kirumba, Alex Ngusa, amewataka
wananchi kutunza vyema mbiundombinu ya barabara inayoendelea kukarabatiwa ikiwa
ni pamoja na kuacha tabia ya kutupa taka kwenye mitaro.
Baadhi
ya wananchi wa Kata ya Kirumba, wamepongeza juhudi za ukarabati wa miundombinu
ya barabara zinazofanyika katika Manispaa ya Ilemela na kuongeza kwamba ni
vyema juhudi hizo zikandelea ili kumaliza kero zilizokuwepo awali.
Mbunge wa Jimbo la Ilemela, yuko katika
mwendelezo wa ziara katika Kata zote 19 za Manispaa ya Ilemela ili kujionea
ukarabati wa Miundombinu ya barabara ambayo ni pamoja na ujenzi wa mitaro na
madaraja ambao unaelezwa kuleta ahueni kwa wananchi wa Manispaa hiy
ikizingatiwa kwamba awali hali ya miundombinu ya barabara awali haikuwa ya
kuridhisha.
"ilemela
ni yetu,tushirikiane kuijenga".
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge.
Jimbo LA Ilemela-Mwanza.
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge.
Jimbo LA Ilemela-Mwanza.
0 comments:
Post a Comment