Katika kuhakikisha
wananchi wa wilaya ya Ilemela wanapata maendeleo ya haraka na yenye tija kwa
kwenda sambamba na kasi ya serikali ya awamu ya tano, Wilaya ya Ilemela
imefanikiwa kupokea wawekezaji kutoka nchini Korea kwa lengo la kuwekeza
wilayani humo hasa kwenye sekta ya viwanda na kilimo.
Hayo yamebainishwa
leo na Ndugu Amos Zephania kwa niaba ya mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa
Ilemela alipokuwa akizungumza na wageni hao kata ya Sangabuye walipokwenda kufanya
upembuzi yakinifu juu ya maeneo sahihi na fursa za uwekezaji zinazopatikana
wilayani humo.
".. Kupitia
wawekezaji hawa wananchi watapata ajira, miundombinu itaimarika sanjari na
kuboresha maisha yao kunakochochewa na upatikanaji wa huduma muhimu za kijamii
kwa uwekezaji huu.." Alisisitiza.
Pamoja na hayo
wawekezaji hao wameahidi kuimarisha mahusiano waliyoyaanzisha na kuwa na tija
kwa pande zote mbili.
Aidha ugeni huu ni
matunda ya ziara ya Mhe Mbunge wa jimbo la Ilemela Dkt. Angeline Mabula alipotembelea
nchini Korea Kusini mapema June 2016 ikiwa ni jitihada za kufungua
milango ya maendeleo ya Jimbo hilo.
"Ilemela ni
yetu,tushirikiane kuijenga"
Imetolewa na
Ofisi ya mbunge
Jimbo la ilemela-mwanza
0 comments:
Post a Comment