Saturday, October 15, 2016

ANGELINE ILEMELA JIMBO CUP YAZIDI KURINDIMA.










Ligi ya Mpira wa Miguu inayojulikana kama Angeline Jimbo Cup imeendelea tena Jimboni humo ambapo timu za Kata ya Nyasaka na Buzuluga zilikuwa zikichuana katika uwanja wa Sabasaba huku mchezo ukimalizika kwa Nyasaka kuichakaza Buzuluga Goli Mbili kwa Sifuri.

Wakati huo huo Timu ya kata Kitangiri imeendelea kuonyesha ubabe dhidi ya Kirumba kwa kuisambaratisha kwa Goli Tatu kwa Moja mechi iliyochezwa uwanja wa Magomeni.

Akizungumza mwanzilishi wa Ligi hiyo ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt. Angeline Mabula amesema kuwa Michezo ni Afya lakini pia Michezo ni Ajira hivyo Vijana wa Jimbo hilo wametakiwa kuitumia fursa hiyo kuonyesha vipaji vyao huku akitolea mifano ya wachezaji mbalimbali wa klabu kubwa nchini waliotokea Jimbo la Ilemela

Nao wananchi waliojitokeza kushuhudia mechi hizo wamemshukuru Mhe Mbunge kwa kuanzisha Ligi hiyo huku wakimuomba kuwepo tena Ligi hiyo kwa mwaka mwengine.

' Ilemela ni Yetu, Tushirikiane kuijenga '

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela~Mwanza


0 comments:

Post a Comment