Jimbo la Ilemela limeendelea
kupata neema ya maendeleo ya haraka na tija kwa watu wake kufuatia maandalizi
ya ugeni mwengine kutoka nchini Korea utakao wasili mapema nchini siku ya
kesho.
Ugeni huo wenye dhamira ya
kuwezesha maendeleo kwa miradi mbalimbali ambayo itapewa kipaumbele na wananchi
wa maeneo husika hasa hasa miradi ya uboreshaji wa makazi ya kuishi na
ujenzi wa vyoo vya kisasa .
Akizungumza katika kikao cha
wenyeviti wa mitaa ya kata za Sangabuye na Kayenze iliyohudhuriwa pia na
wataalamu kutoka Halmashauri ya Manispaa Ilemela Mbunge wa Jimbo hilo na Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dr Angelina Mabula amesema kuwa
wageni hawa ni tofauti na wale wa mwanzo wale ni wawekezaji kutoka Korea na
hawa ni wawezeshaji kutoka nchini Korea, Hawa watajikita katika kujenga
na kuimarisha makazi ya wanachi wa mitaa ya Iponyabugali uliopo kata ya Kayenze
na Ihalalo uliopo kata ya Sangabuye kwa wananchi wenye makazi hatarishi na
wasiokuwa na uwezo wa kuyaboresha.
'…Shughuli za maendeleo
zitategemea sisi wenyewe vipaumbele vyetu kwa kuonyesha ushiriki wetu wa moja
kwa moja anaekusaidia ni lazima aone pale ulipoishia wewe mwenyewe kwanza
hivyo wageni watawasili katika mitaa yetu siku za jumatatu Sangabuye na Jumanne
Kayenze ni wajibu wetu kuwapa ushirikiano wa hali na mali ili waweze kutekeleza
miradi hiyo…'
amefafanua.
amefafanua.
Kwa upande wake Mheshimiwa Naibu
Meya wa Manispaa Ilemela Ramdhan Maganga ameongeza kuwa suala la kujiletea
maendeleo halisubiri kufanywa na watu wa nje ya nchi hivyo wananchi wana wajibu
wa kujitolea kwa hali na mali katika kujiletea maendeleo na kufanikisha miradi
mbalimbali ya Jimbo hilo huku akiahidi ushirikiano kutoka katik ofisi yake na
Halmashauri kwa ujumla .
Nao wenyeviti wa mitaa
inayohusisha miradi hiyo pamoja na viongozi wa kata zao wamemshukuru Mhe
Mbunge wa Jimbo hilo kwa jitihada zake anazozifanya kuhakikisha anatatua
changamoto zote zinazowakabili wananchi wake huku wakiahidi kumpa ushirikiano
kwa miradi yote na shughuli zote za maendeleo zitakazokuja katika maeneo yao.
' Ilemela ni Yetu, Tushirikiane
Kuijenga '
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
0 comments:
Post a Comment