Ile ndoto iliyokuwa ikiotwa miaka yote yakuifanya
michezo kuwa Ajira hatimae yaanza kukamilika Jimboni Ilemela
Hii ni baada ya kuzinduliwa rasmi Leo kwa Ligi ya
Jimbo la Ilemela Kata ya Buswelu ikijumuisha Timu 19 za Mpira wa Miguu
kutoka Kata zote za Jimbo hilo huku uzinduzi huo ukihudhuriwa na Mhe Mkuu wa
Wilaya Ilemela Dr Leonard Masale, Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Madiwani wa
kata mbalimbali na Wananchi
Akizungumza katika Uzinduzi huo Mgeni rasmi
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa Ilemela John Wanga mbali na kumpongeza
Mhe Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dr Angeline Mabula na waandaji wa Ligi
hiyo amewataka Vijana wa Jimbo hilo kukaa mkao wa kula ili kuzitumia
fursa mbalimbali zinazopatikana Jimboni humo ikiwemo ya uwekezaji wa sekta ya
Michezo utakaofanywa na wawekezaji kutoka nchini Korea utakao anza
punde utakao pelekea uzalishaji wa wachezaji wengi na wazuri kwa Timu za ndani
na Nje ya nchi wakitokea Ilemela
Aidha ameongeza kuwa lengo la Halmashauri ni
kuifanya michezo kuwa Ajira, Michezo kuwa Kazi hivyo wananchi wote wanao
wajibu wakuunga mkono jiihada za Serikali na Mhe Mbunge katika kuyafikia
malengo hayo huku akisisitiza nafasi ya Halmashauri, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na
Ofisi ya Mbunge katika kuisaidia Timu ya Wilaya Mbao FC inayoshiriki Ligi Kuu
Tanzania Bara.
Nae Mwakilishi wa Mbunge ambae pia ni
Katibu Ofisi ya Mbunge wa Ilemela Comred Heri James amesisitiza kuwa
Ofisi ya Mbunge itaendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kuwaletea
wananchi maendeleo hasa kupitia Michezo na kuwataka wananchi wa Jimbo
hilo kuwa kitu kimoja na kila mmoja kutimiza wajibu wake katika kuyafikia
maendeleo wanayoyataka
'...michezo ndo dira ya Jimbo hivyo Jimbo Cup iwe chachu ya kuwaleta watu pamoja na umoja wetu ndo mafanikio yetu..' alifafanua.
'...michezo ndo dira ya Jimbo hivyo Jimbo Cup iwe chachu ya kuwaleta watu pamoja na umoja wetu ndo mafanikio yetu..' alifafanua.
Wakihitimisha katika Uzinduzi huo Katibu wa Chama
cha Mpira wa Miguu wilaya ya Ilemela na Diwani Mwenyeji ulipofanyikia uzinduzi
huo Mhe Sara Ng'wani amemshukuru Mhe Mbunge huku akiiomba serikali kuzitafutia
ufumbuzi changamoto za viwanja vya Michezo vilivyopo wilayani humo.
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela~Mwanza
0 comments:
Post a Comment