Halmashauri ya Manispaa Ilemela leo imefanikiwa kufanya
mazungumzo na wawezeshaji kutoka nchini Korea ikiwa ni jitihada katika
kutekeleza sera ya Kijiji cha Maendeleo
Mazungumzo hayo yaliyoanzia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza na
baadae kuishia kwa wananchi wa Kijiji cha Ihalalo kata ya Sangabuye
yaliyohusisha wawezeshaji kutoka nchini Korea, Wananchi, Ofisi ya Mbunge wa
Jimbo la Ilemela na Halmashauri ya Manispaa kama hatua za mwanzo kukifikia
kijiji cha maendeleo.
Wakifafanua kwa wananchi hao wageni hao wamesema kijiji cha
maendeleo ni sera shirikishi iliyosaidia kuleta mageuzi ya haraka kimaisha kwa
watu wa Korea miaka kadhaa iliyopita hasa maeneo ya Vijijini huku ikijumuisha
nguvu kubwa ya wananchi wenyewe na vipaumbele vyao katika kujikwamua kimaisha.
Akizungumza mbele ya wananchi wa Ihalalo Katibu Ofisi ya Mbunge
wa Jimbo la Ilemela Ndugu Heri James amesema kuwa ndoto ya Mbunge wa Jimbo hilo
ni kuiona Ilemela katika Kilele cha mafanikio huku akitanabaisha kuwa hayo
hayatafanikiwa kama ushirikiano wa wananchi hautakuwepo
"…Mbunge wenu anafanya jitihada kubwa mchana na usiku kuhakikisha anawaletea maendeleo na haya ya leo ni matokeo ya Ziara yake Lakini sisi kama wananchi tujue tuna la kufanya na wajibu wetu kila tutalopanga kulifanya tuwe wa kwanza kulitekeleza…''
Aidha Mstahiki Meya wa Manispaa Ilemela ambae pia ni Diwani wa
Kata ya Mradi Mhe Renatus Mulunga amewashukuru wageni hao kwa kuamua kuanzisha
Kijiji cha Maendeleo huku akiwahakikishia ushirikiano wa Halmashauri katika
kufanikisha mradi huo kwa wananchi.
Nao wananchi wa Ihalalo wameishukuru Serikali na Ofisi ya Mbunge
kwa jitihada mbalimbali wanazozifanya kuhakikisha wananchi wanapata
maendeleo huku wakiahidi ushirikiano wao wa hali na mali kukifikia Kijiji
cha Maendeleo.
"Ilemela ni yetu,tushirikiane kuijenga"
Imetolewa na
Office ya mbunge
Office ya mbunge
Ilemela-Mwanza
0 comments:
Post a Comment