Katika juhudi zake za
kuimarisha mchezo wa soka Jimboni na kukuza dhana ya michezo ni ajira Mhe
Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Dkt. Angeline S L Mabula amegawa vifaa vya michezo kwa timu 19 kutoka
katika kila kata za Jimbo.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa
Maafisa Watendaji na Viongozi wa Timu kutoka kila Kata kwa niaba ya Mhe Mbunge,
Katibu wa Ofisi ya Mbunge Comred Kheri James amesema Mhe Mbunge ana ndoto ya
kuwaona Vijana wa Ilemela wanastawi kiuchumi kupitia mpira wa miguu kwa kuwa
wachezaji bora wa ndani na nje ya nchi yetu.
Vifaa hivi vimegawiwa ikiwa ni sehemu ya
maandalizi ya ligi ya jimbo "ANGELINE JIMBO CUP" inayo tarajiwa
kuanza jumanne wiki ijayo kwa kuzinduliwa rasmi katika kiwanja cha Buswelu na
kuhudhuriwa na Viongozi, Wananchi, na Timu za Kata zote zitakazo shiriki katika
Ligi hii ilio andaliwa na Mhe Mbunge.
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela~Mwanza
0 comments:
Post a Comment