Mbunge wa Jimbo la Ilemela na
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Daktari Angeline Mabula
ametekeleza ahadi yake aliyoitoa katika kipindi cha kampeni kwa kuhakikisha
anainua na kuboresha kiwango cha Elimu Jimboni humo ikiwa ni pamoja na kuzisaidia
Shule zote zinazofanya vibaya wilayani huko ili kutoa fursa sawa kwa kila mtoto
hasa masikini kufikia ndoto zake
Katika kuhakikisha hili linafanikiwa Mbunge huyo leo ametoa
vitabu 720 vya masomo ya Sayansi pamoja na kusaidia utatuzi wa baadhi ya changamoto
zinazokabili Shule hizo za Sekondari Jimboni Ilemela kwa kuanza
kuzitembelea Shule za mfano kama Mihama Sekondari iliyopo Kata Kitangiri,
Kilimani sekondari iliyopo Kata Kawekamo na Ibinza iliyopo Kata Nyamhongoro
Akimkaribisha Mheshimiwa Mbunge Katibu wa Ofisi ya Mbunge
huyo Comred Heri James ameeleza kuwa kumekuwepo na utaratibu wa kupongeza
Shule zinazofanya vizuri ila Jamii na Viongozi wamekuwa hawana utaratibu wa
namna gani wanawatia moyo na kusaidia Shule zote zinazofanya vibaya kitaaluma,
Hivyo basi Mheshimiwa Mbunge wa Ilemela amefungua Ukurasa mpya katika
kuziwezesha Shule zote zilizo chini kitaaluma ndani ya Jimbo hilo kuanza
kufanya vizuri Kimkoa na Kitaifa
Nae Mbunge wa Jimbo hilo amesema kuwa kwa kipindi chote cha
Uongozi wake atahakikisha anashirikiana na wananchi naTaasisi nyengne zozote
ili kuleta Maendeleo ya moja kwa moja kwa Wananchi wa Ilemela huku akiwataja
Bwana Steve na Bi Judith walioshirikiana na Taasisi ya Angeline Foundation
katika kusaidia upatikanaji na Ugawaji wa vitabu hivyo
Mbunge ameendelea kwa kusema kuwa katika kampeni zake aliahidi
kuzipa zawadi Shule zote zitakazofanya vizuri lakini akaona kuwa
inawezekana wanaofanya vibaya ni sababu ya kukosekana kwa baadhi ya vitendea
kazi kama vitabu na kuona ipo haya ya kuitatua changamoto hiyo katika safari ya
Tanzania ya Viwanda
'… Kuzidisha wataalamu wa masomo ya Sayansi nadhani ndo
tumeianza safari ya katika kuifikia Tanzania ya Viwanda kwani tutakuwa na
wataalamu wa kutosha waliosoma masomo ya sayansi watakaosaidia viwanda hivyo…'
Wakati huo huo Mheshimiwa Mabula amemwomba Afisa Elimu wa
Halmashauri ya Ilemela Mwalimu Kasandiko kuanza kuzitumia Chaki alizozitoa Mkoa
Simiyu zinazojulika kama MASWA CHALKS kama majaribio na baadae kutumika kwa
Wilaya nzima kama hazitakuwa na Tatizo lolote ili kukuza na kutoa fursa ya
kukua kwa bidhaa zinazozalishwa na Viwanda vya ndani
Akihitimisha Afisa Elimu wa Manispaa Ilemela amemshukuru Mbunge
huyo na kusema kuwa amekuwa Mbunge wa kuigwa kwani mara zote yupo Jimboni kwa
shughuli za kimaendeleo na kumhakikishia ushirikiano katika kuboresha Elinu kwa
wilaya hiyo..
“Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga”
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
25/11/2016
0 comments:
Post a Comment