Mbunge wa Jimbo la Ilemela na
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
ameendelea na jitihada za kuhakikisha anawatumikia wana Ilemela na kuwaletea
maendeleo ya haraka.
Mhe Dkt Mabula leo
amekutana na Balozi wa Korea nchini Tanzania na kufanya nae mazungumzo yenye
lengo la kuimarisha mahusiano baina ya Manispaa ya Ilemela na Jiji la Daegu
lililopo nchini Korea sambamba na mazungumzo juu ya Timu ya Wataalamu,Viongozi
na Wananchi wa Ilemela waliokwenda nchini Korea hivi karibu kwaajili ya mafunzo
ya uwekezaji na uwezeshaji inayoongozwa na Mhe Mstahiki Meya wa Manispaa
hiyo Renatus Mulunga.
Mhe Dkt Mabula pia
ameitumia fursa hiyo kumkabidhi Balozi wa Korea andiko la
mradi kwaajili ya kuwasaidia wananchi wanaofanya shughuli za ujasiliamali
kwenye maeneo ya mialo
' Ilemela ni yetu,Tushirikiane kuijenga '
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
0 comments:
Post a Comment