Makamu wa Rais Samia Suluhu leo amezindua Jengo
la Utawala na Uzio wa Halmashauri ya Manispaa Ilemela pamoja na kugawa Madawati
kwa Manispaa hiyo ikiwa ni muendelezo wa Ziara yake Mkoani Mwanza
Katika hotuba yake kwa mamia ya Wananchi na
Viongozi mbalimbali waliojitokeza kwenye Uzinduzi huo Mheshimiwa Makamu wa Rais
ameeleza kuwa anafurahishwa na kasi ya utekelezaji wa shughuli za kimaendeleo
ndani ya Jimbo la Ilemela na kumpongeza Mbunge wa Jimbo hilo huku akiwaasa
wananchi wa Ilemela kumtumia Vizuri Mbunge huyo ambaye Pia ni Naibu Waziri wa
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
'… Mna Mbunge Mzuri naamini mkimtumia vyema atawasaidia katika kuipanga Vizuri Ilemela…'
Katika kuvutiwa na Kauli mbiu ya Wilaya Ilemela
inayosema kuwa ILEMELA NI YETU TUSHIRIKIANE KUIJENGA Mhe Makamu wa Rais
ameongeza kuwa Maendeleo ya sehemu huletwa na watu wa eneo lile kwa
kufanya Kazi kama Kauli Mbiu ya Serikali inavyosema HAPA KAZI TU
Aidha Mhe Makamu wa Rais amesema kuwa atapendezwa
iwapo Kauli Mbiu hiyo itakuwa Kauli Mbiu ya Mkoa na kuongeza kuwa atakuwa Mlezi
wa Wilaya Ya Ilemela kufuatia kufurahishwa kwake na Kasi hiyo ya Utekelezaji wa
Shughuli za kimaendeleo
Akimkaribisha Makamu wa Rais Mkuu wa Mkoa Mwanza
Mhe John Mongella amemuhakikishia Makamu huyo kuwa Kasi ya Maendeleo ya Ilemela
ni kubwa na kusema kuwa wasipobweteka na kuongeza Juhudi itakuwa Wilaya ya
Mfano ndani ya nchi yetu
Nae Mbunge wa Jimbo hilo na Naibu Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Daktari Angeline Mabula mbali na kuwapongeza
Mhe Rais na Makamu wake amemshukuru Makamu wa Rais na kuahidi kuwa kama Mteule
wa Rais atahakikisha anatekelza Ilani ya Chama kama inavyoelekeza kwa
kushirikiana na Wananchi kama Kauli Mbiu inavyoelekeza huku akifafanua juu ya
utengenezaji wa madawati 1000 yaliyotokana na nguvu za wananchi na kumuomba
kutoa msaada pale itapohitajika
'… Wewe ni Mama na Mimi ni Mama Pale tunapoomba Msaada tunakuomba utuunge Mkono…'
Imetolewa Na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
18.11.2016
0 comments:
Post a Comment