MBUNGE WA ILEMELA ALIPONGEZA KANISA KATOLIKI KWA KUSAIDIA MAENDELEO YA JAMII.
Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Daktari Angeline Mabula leo
ameshiriki mahafali ya Shule ya Sekondari ya Mtakatifu Maria iliyopo Nyegezi
Malimbe ikiwa ni utekelezaji wa majukumu yake katika kuhakikisha anawatumikia
wananchi wote na kuleta chachu ya maendeleo kwa wananchi
Akihutubia mamia ya wazazi na wanafunzi
waliohudhuria mahafali hayo Mhe Mabula amelishukuru Kanisa Katoriki kwa
kuisaidia Serikali katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo huku
akiwahakikishia kuwa Serikali itaendelea kutatua changamoto za Ardhi kwa
taasisi mbalimbali za kidini
Aidha Mhe Angeline Mabula amewakumbusha wanafunzi
wa shule hiyo kuyaishi maisha ya Seminari kwa kipindi chote cha maisha yao
wakati huu wanapoondoka shuleni na kuyaendeleza mafundisho waliyoyapata
shuleni hapo
'…Seminari ni Tanuru la wito, Seminari ni sehemu
ya kuzalisha wahudumu wa kanisa ni lazima kuyaishi maisha ya Seminarini huko
muendako…'
Akimkaribisha Mgeni rasmi huyo Baba Askofu wa
Jimbo kuu la Mwanza Yudathadei Rwaichi amemshukuru Mbunge huyo huku
akimuhakikishia juu ya shule hiyo kuendelea kutoa elimu kwa kuzingatia Masomo,
Kazi, Sala na Michezo huku Mkuu wa Shule hiyo akielezea namna Seminari hiyo
inavyofanya vyema Kimkoa na Kitaifa
Mahafali
hiyo imehudhuriwa pia na Mh.mbunge wa jimbo la Nyamagana Mh.Stanislaus
Mabula,mbunge wa Magu Mh.Kiswaga,Mh.Maria Kangoe,waheshimiwa madiwani na
viongozi wa chama walioongozwa na m/kiti wa uwt mkoa wa Mwanza Mh.Hellen Bogohe
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
19.11.2016
0 comments:
Post a Comment