Saturday, November 19, 2016

MBUNGE WA ILEMELA AHITIMISHA FAINALI ZA ANGELINE ILEMELA JIMBO CUP











Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa Daktari Angeline Mabula amehitimisha mashindano ya mpira wa miguu yaliyohusisha Timu za kutoka Kata zote zilizopo ndani ya Wilaya ya Ilemela yaliyojulikana kama Angeline Ilemela Jimbo Cup yaliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Vyama vya Siasa na Serikali yaliyofanyika Uwanja wa CCM Kirumba

Angeline Ilemela Jimbo Cup iliasisiwa na Mbunge wa Jimbo la Ilemela kwa Lengo la Kukuza Vipaji mbalimbali vya Michezo vinavyopatikana ndani ya Jimbo hilo na kuifanya Michezo kuwa Ajira na yenye tija kwa Jamii ya Ilemela na Taifa kwa Ujumla wake

Fainali za Angeline Ilemela Jimbo Cup zilihusisha Timu za Kata ya Bugogwa na Kata ya Ibungilo ambapo Timu ya Kata Bugogwa ilianza kwa kuijeruhi Timu ya Kata Ibungilo kwa magoli 2 kwa  0 kabla ya Mshambuliaji Jezi namba 11aliyejulikana kwa jina la Andrea kuipatia goli la kwanza Timu yake  mpaka Dakika 90 ya mchezo huo ikimalizika kwa Timu zote kutoka Sare ya Magoli 3 kwa 3 na mwishowe mchezo kumalizika kwa Timu ya Bugogwa kuigaragaza Timu ya Ibungilo kwa mikwaju ya Penati ya goli 1 kwa 0, Wakati Timu ya Kata Kitangiri ikiibuka Mshindi wa Tatu kwa kuichapa Timu ya Kata Shibula magoli 2 kwa 0

Akizungumza katika Mchezo huo Mbunge wa Ilemela na muasisi wa Angeline Ilemela Jimbo Cup
Mheshimiwa Angeline Mabula amesema kuwa Uwepo wa Ligi hiyo ni Utekelezaji wa Ahadi yake alioitoa kwa Wananchi wake  kipindi cha Uchaguzi katika kuhakikisha anaboresha michezo yote na kuibua Vipaji vipya vinavyopatikana ndani ya Jimbo hilo huku akiifanya Michezo kuwa Ajira
'…Hii ni Ahadi yangu ya Kipindi cha Uchaguzi katika kuibua Vipaji vipya Ilemela na kuifanya Michezo kuwa Ajira kwa Vijana wetu...'

Nae Waziri wa Habari na Michezo Mheshimiwa Nape Nnauye amempongeza Mbunge wa Ilemela kwa kuasisi Ligi hiyo pamoja na hatua mbalimbali anazochukua katika kukuza Michezo huku akiahidi kumuunga mkono mapema mwakani itakapoanza tena Ligi hiyo
Wakati huo huo Waziri huyo ameahidi  Laki Mbili kwa kila Goli litakalofungwa kupitia fainali hizo kwa mshindi

Aidha Mshindi wa Kwanza wa Fainali hizo alijinyakulia  Kitita cha Shilingi Milioni moja, Seti Moja ya Jezi na Kikombe huku Mshindi wa Pili akipata Kitita cha Laki Tano, Seti Moja ya Jezi na Kikombe na Mshindi wa Tatu akiambulia Laki Tatu, Seti Moja ya Jezi na Kikombe

'…Ilemela ni Yetu, Tushirikiane kuijenga…'


Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela~Mwanza

0 comments:

Post a Comment