Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Daktari Angeline Mabula leo amehudhuria
Mahafali ya Pili tangu kuanzishwa kwa Shule ya Sekondari ya
Wasichana Holyfamily iliyopo Kata ya Mkolani Nyamagana Mwanza katika
kuhakikisha anawatumikia waTanzania wote na kuhamasiha maendeleo na tija kwa
Taifa
Pamoja na kutoa salamu kutoka kwa Mbunge wa
Nyamagana kwa hadhara hiyo Daktari Angeline Mabula amewaasa wanafunzi hao
kuyaendeleza maadili na misingi mema waliokuwa nayo shuleni huku akiwafafanulia
umuhimu wao na utegemezi wa Taifa kwa kuwataka kuziishi ndoto zao kwa
vitendo sanjari na kuwakumbusha wajibu wa wazazi kwa watoto katika suala zima
la kuisaidia serikali kutimiza lengo la kutoa Elimu Bure na yenye manufaa kwa
wananchi wote
Aidha Mheshimiwa Daktari Mabula amewataka
wahitimu waliokwisha nufaika na mikopo ya Elimu ya Juu kulipa madeni yao
ili kutoa fursa kwa vijana wengine masikini waweze kunufaika na mwisho kufikia
malengo yao kwa kupata Elimu bora
'…Lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi wake wanapata Elimu bora na kwa unafuu lakini niwatake wale waliokwisha nufaika na mikopo ya Elimu ya Juu kulipa madeni yao ili na wengine waweze kunufaika, Suala la Elimu bure halimaanishi kuwa mzazi huna wajibu katika kumpatia mtoto Elimu bora wazazi na walimu kwa pamoja tunaowajibu katika kufikia malengo na sera ya Serikali katika kuitoa hii Elimu bure kwa kutimiza wajibu wetu…'
Akizungumza Mwenyekiti wa bodi ya Shule Ndugu
Luvulilo Elisha Pamoja na Kumshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri Daktari
Angeline Mabula amewaasa wanafunzi wa Shule hiyo kuiga mfano wa Mgeni rasmi
huyo kwa kuwa mwanamke jasiri, mpenda maendeleo, anaeweza kujisimamia na
mwenyekuandika historia kwa kuwa mwanamke wa kwanza kuwa Mbunge wa Jimbo kwa
kuchaguliwa tangu kuanzishwa kwa Jimbo la Ilemela
'..Huyu ni mwanamama Jasiri, mwanamama anayejisimamia, mwanamama mpenda maendeleo hivyo nawataka wanafunzi nyinyi mnaohitimu leo kuiga mfano wake kwa kuendeleza pale wanapoishia wanawake wenzenu..' alisisitiza
Nae mwanafunzi Edith Lugela aliyepata zawadi ya
kuwa mwanafunzi bora wa Shule hiyo kwa mwaka huu na kutwaa tuzo ya malikia wa
shule amemshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri Mabula kwa moyo wake wa kujitoa kwa
jamii inayomzunguka hasa katika kuhakikisha jamii inajikwamua na kujiletea
maendeleo.
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela Mwanza
12.11.2016
0 comments:
Post a Comment