Jimbo la Ilemela limekabidhiwa gari aina ya
Toyota Land Cruiser na Serikali kuu ikiwa ni hatua katika kuboresha huduma za
Afya kwa wananchi wa Jimbo la Ilemela
Aidha magari ya aina hiyo yamekabidhiwa kwa
wabunge wanaotoka majimbo ya kanda ya Ziwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa
Jamii Mhe Ummy Mwalimu ikiwa ni muendelezo wa Juhudi za Serikali ya awamu
ya Tano katika Kuboresha huduma za Afya na Jamii
Akipokea gari hilo Mbunge wa Jimbo la Ilemela na
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula ameishukuru
Serikali kwa kuamua kugawa magari hayo yatakayosaidia kuboresha huduma za
Afya hasa kwa mama na mtoto huku akiiomba kufanya hivyo kwa sekta nyenginezo za
huduma za kijamii ili kusaidia wananchi masikini kumudu gharama za kupata
huduma muhimu
Wakati huo huo Mbunge akimkabidhi gari hilo
Mganga Mkuu wa Manispaa Ilemela ndugu Wilfred Rwechungura amemtaka kulitunza na
kuhakikisha linafanya shughuli iliyokusudiwa
Gari hilo litapelekwa kituo cha Afya Sangabuye
kinachokabiliwa na changamoto kubwa ya Usafiri wa kubebea wagonjwa hasa
inapotokea dharula
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
0 comments:
Post a Comment