Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amefanya Ziara kwa Kata ya
Buzuluga ikiwa ni muendeleo wa Ziara yake kwa kata zote 19 zilizomo
ndani ya Jimbo la Ilemela katika kuwasikiliza wananchi, kutatua kero
zinazowakabili sambamba na kuwahamasiha juu ya utendaji wa shughuli
mbalimbali za kimaendeleo
Katika ziara hiyo Mhe Mbunge ameambata na Mkuu wa wilaya
Ilemela, mkurugenzi na Wakuu wa Idara za Manispaa Ilemela ili kuweza
kubainisha changamoto zinazowakabili wananchi na kuzipatia majawabu ya
papo kwa hapo
Akizungumza katika Ziara hiyo Mhe Mbunge amewahimiza
wananchi wa kata Buzuluga juu ya kuwa wamoja na kushirikiana katika
kutatua changamoto za kata hiyo sambamba na kuwataka kuacha kujenga bila
ya kufata taratibu ili kuruhusu huduma nyengine za kijamii kuendelea
pamoja na kuitumia fursa ya urasimishaji wa makazi na upangaji mji ili
kuongeza thamani ya ardhi waliyonayo na si kuuza mashamba tupu
'… Ili kazi ziende ni lazima tushirikiane Sisi, mkuu wa
wilaya, Mkurugenzi na Meya tunashirikiana lakini msikubali kuuza
mashamba uzeni viwanja vilivyokwishapimwa na kupewa hati ili kuongeza
thamani ya viwanja vyenu…'
Akimkaribisha Mbunge huyo Mkuu wa wilaya Ilemela mhe Dkt
Leonard Masale mbali na kumshukuru kwa jitihada zake za kila siku katika
kuhakikisha anawatumikia wana Ilemela amewataka wazazi na watendaji wa
wilaya hiyo kushirikiana katika kutatua changamoto zinazoikabili sekta
ya Elimu wilayani humo na si kuiachia serikali pekee huku akiwataka
machinga wa wilaya hiyo kuanzisha Umoja wao utakao kuwa na Uongozi ili
iwe rahisi kupata msaada kutoka serikalini tofauti na kumsaidia mtu
mmoja mmoja
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa Ilemela Mhe John
Wanga pamoja na kujibu maswali yote yanayohusu Manispaa yake kwa
wananchi amewataka viongozi wa mitaa kuwa sehemu ya utatuzi wa migogoro
ya ardhi katika maeneo yao na kuwa mstali wa mbele katika kuleta
maendeleo huku akisisitiza ushirikiano na umoja kwa wadau wote wa
maendeleo
Ziara ya Mhe Mbunge itaendelea tena leo kata ya Mecco
' Ilemela ni yetu, Tushirikiane kuijenga '
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
17.12.2016
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
17.12.2016
0 comments:
Post a Comment