Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula Leo amekutana na Vijana wa Ilemela
wanaoichezea Timu ya Mpira wa miguu ya Vijana nchini
Serengeti Boys
Timu ya Wavulana Serengeti Leo imefanya Ziara ya kutembelea
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma.
Akizungumza na Wageni hao Mbunge wa Ilemela amewahakikishia
kuendeleza ushirikiano katika kukuza Michezo ndani ya Jimbo na nje ya
Jimbo huku akiwapongeza kwa mafanikio na heshima waliyoiletea Taifa
sambamba na kuwataka kuacha kubweteka na kuongeza juhudi ili kupata mafanikio
zaidi ya waliyonayo sasa.
Hivi karibuni Mbunge wa Ilemela mbali na kufanya kampeni ya
kukuza Elimu ameendeleza kampeni ya kuhakikisha anakuza vipaji vya michezo
mbalimbali jimboni kwake kwa kuanzisha Angeline Ilemela Jimbo Cup na Maazimisho
ya kumkumbuka aliyekuwa mchezaji wa Mbao Fc Ismail Mrisho ikiwa ni mkakati wa
kuifanya Michezo kuwa Ajira.
Jumla ya wachezaji wapatao Wanne wanaotoka Jimbo la Ilemela
wamepata fursa ya kuichezea Timu ya Vijana ya Taifa Serengeti wakiwemo Ally
Hussein, Israel Patrick, Ally Hamis na Kelvin Nashon.
Wakati huo huo Mhe Mabula ameendelea kuwawakilisha vema wananchi
wa Jimbo la Ilemela jioni ya Leo katika vikao vya Bunge vinavyoendelea mjini
Dodoma.
' Ilemela ni yetu, Tushirikiane kuijenga '
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
09.02.2017
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
09.02.2017
0 comments:
Post a Comment