Mbunge wa Jimbo la
Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline
Mabula amekutana na kufanya mazungumzo na Shirikisho la Vyama vya Walemavu
Tanzania SHIVYAWATA ofisini kwake jijini Dar es Salaam
Akizungumza na
SHIVYAWATA Mhe Mabula amesema kuwa amefurahishwa na Jitihada wanazozifanya
katika kuhakikisha Walemavu wanaondokana na utegemezi kwa kujishughulisha na
miradi mbalimbali ya kujikwamua kiuchumi huku akiwahakikishia kuwa Serikali ya
Awamu ya Tano inalitambua kundi hilo na kuahidi kuendelea kuwaunga mkono kwa
kila wanachofanya
Nae Mwenyekiti wa
SHIVYAWATA Bi Ummy Nderinga ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa
na Mhe Rais Dkt John Magufuli kwa hatua
mbalimbali wanazozichukua katika kuwasaidia watu wenye ulemavu huku akiwataka
viongozi wengine na Jamii kiujumla kuiga mfano wa Dkt Mabula katika kuunga
mkono jitihada za kuwasaidia walemavu nchini
'... Tunaishukuru
Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuendelea kuisaidia jamii ya watu wenye ulemavu
naomba sana na wengine waige mfano wa Naibu Waziri Mabula kwa kuunga mkono
jitihada za wenye ulemavu...'
Aidha Mwenyekiti
Nderinanga ameongeza kuwa lengo la mazungumzo yao ni kuhakikisha SHIVYAWATA
inapata maeneo rafiki kwajili ya ujenzi wa Ofisi na Maeneo kwaajili ya uendeshwaji
wa Miradi mbalimbali yenye lengo la
kumsaidia mlemavu aweze kujikwamua kiuchumi na kujitegemea
'...Ilemela ni yetu, Tushirikiane
kuijenga...'
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
14.02.2017
0 comments:
Post a Comment