Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ndo
Mlezi wa Halmashauri ya Manispaa Ilemela Mheshimiwa Samia Suluhu amefanya Ziara
Ilemela ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa mapema mwishoni mwa mwaka
jana wakati wa ufunguzi rasmi wa Jengo la Halmashauri ya Manispaa hiyo
Akizungumza katika mkutano uliojumuisha Viongozi mbalimbali wa
ngazi za mitaa, kata, wilaya, Mkoa na watumishi wa Manispaa hiyo Mheshimiwa
Samia mbali na kutoa Pongezi kwa jitihada za kimaendeleo zinazofanywa ameitaka
Ilemela kuanzisha mikakati katika kupambana na vita ya madawa ya kulevya ,
uvuvi haramu sambamba na uanzishwaji wa jukwaa la wanawake lenye lengo la
kumwezesha mwanamke kujikwamua kiuchumi na kutatua changamoto zinazowakabili
'... Niliahidi nikikanyaga Mwanza ni lazima nifike Ilemela na
hii ni kwasababu Ilemela mpo teyari kwa kazi inayojidhihirisha kwa mafanikio
mliyoyapata hasa kwenye sekta ya Elimu...'
Akimkaribisha Makamu wa Rais Mkuu wa Mkoa Mwanza
Mheshimiwa John Mongela amemuhakikishia kuwa anaridhishwa na kasi ya maendeleo
inayofanywa na Ilemela sambamba na hatua nzuri katika ukusanyaji wa mapato
'... Ilemela ni miongoni mwa Halmashauri tegemezi kwa Mkoa wetu
katika ukusanyaji wa mapato hivyo niwapongeze sana Madiwani, Mkurugenzi na
watendaji wote kwa utendaji kazi wao katika kuleta mabadiliko...'
Akisoma taarifa yake Mkurugenzi wa Ilemela John Wanga kwa niaba
ya Mkuu wa wilaya hiyo Daktari Leonard Masale mbali na utekelezaji wa Maagizo
ya Mheshimiwa Makamu wa Rais aliyoyatoa katika Ziara yake ya awali amemuomba
kuisaidia Manispaa hiyo juu ya umaliziaji wa miradi yake ya maji, barabara,
ulipaji wa fidia za ardhi na hospitali jambo ambalo Mlezi huyo aliahidi
kulifanyi kazi
Akihitimisha Mbunge wa Jimbo hilo na Naibu Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Daktari Angeline Mabula amemshukuru Mheshimiwa
Makamu wa Rais kwa Uamuzi wake wa kuzuru Ilemela na kumsisitiza kutomchoka kwa
kipindi chote atakachokuwa akimsumbua katika kuhakikisha wanaungana katika
kuletea maendeleo ya Ilemela
'... Ilemela ni yetu, Tushirikiane kuijenga...'
Imetolewa na
Ofisi ys Mbunge
Jimbo la Ilemela
16.02.2017
Ofisi ys Mbunge
Jimbo la Ilemela
16.02.2017
0 comments:
Post a Comment