Aliyekuwa Balozi wa Korea
Kusini nchini Tanzania kuanzia mwaka 2009 hadi 2012 Mheshimiwa Balozi Kim,
Young-hoon amemtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma Mbunge wa Jimbo la Ilemela
na Naibu Waziriwa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Daktari Angeline Mabula
lengo likiwa ni kuimarisha mahusiano baina ya Ilemela na Miji rafiki ya nchini
Korea, Kufungua zaidi fursa za Uwekezaji baina ya nchi hizo na
utekelezaji wa miradi yote ya kimaendeleo inayotaraji kuanza Jimboni humo
muda wowote kutoka sasa.
Mbali na Balozi huyo Timu ya Uwekezaji ijulikanayo kama KICOT
inayojumuisha waTanzania na Wakorea imeambatana na Balozi huyo katika Ziara
hiyo huku ikimjumuisha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa Ilemela Ndugu John
Wanga, Ndugu Son, Ndugu Kim, Ndugu Lee Kwang Se, Ndugu Lee
Jae-Yong na Ndugu David Mabula .
Aidha ugeni huu unataraji kuwasili jijini Mwanza, Ilemela
mapema jioni ya leo kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo
kufuatia kusainiwa kwa mikataba mbalimbali ya miradi ya shughuli za maendeleo
mapema mwishoni mwa mwaka jana.
' Ilemela ni yetu, Tushirikiane kuijenga'
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
05. 04. 2017
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
05. 04. 2017
0 comments:
Post a Comment