Wednesday, April 5, 2017

UGENI WA WAWEKEZAJI KUTOKA NCHINI KOREA WAWASILI RASMI NCHINI





Ile ndoto ya kuifikia Ilemela yenye neema ya mafanikio inaelekea kutimia kufuatia kuwasili kwa ugeni wa wawekezaji kutoka nchini Korea Kusini uliowasili mapema nchini kwa kuanza utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya Manispaa ya Ilemela .

Ikumbukwe kuwa kuwasili kwa ugeni huu kunakuja kufuatia ziara aliyoifanya Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi mapema  mwaka Jana na baadae Viongozi wa Manispaa Ilemela wakiongozwa na Meya wa Manispaa hiyo Mheshimiwa Renatus Mulunga akiambatana na Mkurugenzi wake John Wanga kwa kuitembelea miji rafiki ya nchini Korea kwa lengo la kubadilishana uzoefu, kuingiwa kwa mikataba mbalimbali ya shughuli za maendeleo na Uwekezaji.

Kabla ya kuwasili wilayani Ilemela hapo siku ya alhamisi kwa utekelezaji wa shughuli za kimaendeleo  Ugeni huu wa Uwekezaji hapo kesho siku ya jumatano unataraji kukutana na Viongozi wa Wizara ya fedha, Wizara ya Majii na Umwagiliaji na baadae Wizara ya Afya

  '... Ilemela ni yetu,Tushirikiane kuijenga ...' 


Imetolewa na  
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
04.04.2017

0 comments:

Post a Comment