Miradi mbalimbali ya Uwekezaji inayotaraji
kufanyika ndani ya Jimbo la Ilemela itakuwa fursa ya kukuza uchumi wa wananchi
wa jimbo hilo.
Hayo yamebainishwa na balozi mstaafu wa Korea katika mazungumzo
yake na viongozi wa Ilemela akiwemo Mkuu wa wilaya Ilemela Mhe Dkt Leonard
Masale, Meya wa Manispaa Ilemela Mhe Renatus Mulunga, Naibu Meya Mhe Shaban
Maganga, Kaimu Mkurugenzi Mhe Daniel Batare, Katibu Ofisi ya Mbunge Heri James,
wataalamu wa Manispaa Ilemela na wageni
alioambata nao kutoka nchini Korea.
Aidha Ugeni huo wa uwekezaji ulianza kwa kufanya
kikao kifupi na mkuu wa mkoa Mwanza Mhe John Mongela na baadae kutembelea
maeneo yaliyotengwa kwa utekelezaji wa
miradi yakiwemo Ihalalo, Nyamhongolo, eneo la mafunzo ya kilimo chini usimamizi
wa The Angeline Foundation Imalang'ombe na shule ya sekondari wavulana Bwiru.
Balozi huyo mstaafu wa Korea Kim Young Hoon amesema
kuwa anafurahishwa na kasi ya maendeleo ya Jimbo la Ilemela na kuongeza ni matumaini yake kuona miradi ya uwekezaji
itayotekelezwa ikileta manufaa ya kukua kwa uchumi wa pande zote mbili .
'... Nafurahishwa na kasi ya ukuaji wa mji wa
Ilemela sambamba na ushirikiano kutoka wa muasisi wa mahusiano ya pande hizi
mbili chini ya Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula , Matumaini yangu kuona uwekezaji
tunaoufanya ukichochea ukuaji wa uchumi kwa wananchi wetu...' Alisema .
Nae mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe Dkt Masale na
Meya wa manispaa hiyo Mhe Mulunga mbali
na kushukuru kwa maamuzi yao ya kuichagua Ilemela kama eneo la uwekezaji
wamemuhakikishia ushirikiano wa utekelezaji wa makubaliano yote katika
kufanikisha utekelazi wa miradi hiyo huku wakihimiza mawasiliano ya Mara kwa
mara.
Akihitimisha Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Ilemela
Ndugu Heri James amesema
'... Mengi mmezungumza na Dkt Mabula Sisi kazi yetu ni kusisitiza na
tunawahakikishia utayari na umakini katika kufanikisha dhamira ya uwekezaji na
tunaamini bado tuna mengi yakufanya kwa pamoja ...'
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
07.04.2017