Thursday, August 18, 2016

MBUNGE WA JIMBO LA ILEMELA ATOA VIFAA VYA MICHEZO.












Katika kuhakikisha ndoto za vijana wengi zinatimia hasa wale wanaojihusisha na michezo Mbunge wa Jimbo la Ilemela-Mwanza na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba, na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline.S.L.Mabula ametoa vifaa vya michezo kwa shule ya wavulana ya Bwiru ikiwa ni kutimiza ahadi yake alioitoa kwa wanafunzi wa shule hiyo kutokana na ombi la wanafunzi hao alipo watembelea shuleni hapo wiki mbili zilizopita.

Akikabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya Mh. Mbunge, katibu wa ofisi ya mbunge jimbo la Ilemela Komred Kheri James amewasihi wanafunzi kivitumia vyema vifaa hivyo ili kujiimarisha katika michezo na kuwa na ndoto ya kuwa wanamichezo wasomi watakao badili mwelekeo wa michezo hapa nchini na kuzidi kupanua dhana ya michezo katika wigo wa afya na uchumi.

Pamoja nakukabidhi vifaa hivyo Mhe Mbunge ametoa pole kwa mkuu wa shule ya wavulana  Bwiru  ambae ni mgonjwa na anaendelea na matibabu katika hospitali ya mkoa wa Mwanza.

"ILEMELA NI YETU TUSHIRIKIANE KUIJENGA"                  
Imetolewa;
Ofisi ya mbunge ilemela-Mwanza
                                  

0 comments:

Post a Comment