Katika hali ya kukutana na makundi na watu mbalimbali ndani ya jimbo,Mh
Mbunge wa jimbo la Ilemela Dkt.Angeline.S.L.Mabula amemtembelea nyumbani
kwao msanii Jet Man ambae ameugua kwa takribani miaka mitano bila kuamka
kitandani kutokana na tatizo la kupooza sehemu ya mwili.
Akiwa nyumbani hapo mh.Mbunge amempa pole msanii huyo na kuahidi
kushirikiana na watu wengine waliojitolea ktk jamii kusaidia matibabu ya msanii
huyo.Mh.Mbunge amesaidia vifaa na mahitaji mbalimbali ili kumsaidia japo kwa
uchache ndugu yetu huyo.Jet Man ni miongoni mwa vijana wa Ilemela walio vuma
saana ktk mziki wa kizazi kipya ktk siku za nyuma.
Niimani yetu kila mmoja wetu akiguswa na tunaweza kumsaidia Jet Man
kurejea ktk afya yake.
"Ilemela ni yetu,tushirikiane kuijenga".
Imetolewa na.
Ofisi ya mbunge.
Jimbo la Ilemela-Mwanza
0 comments:
Post a Comment