Thursday, March 9, 2017

MBUNGE WA JIMBO LA ILEMELA ATUNUKIWA TUZO YA UONGOZI BORA






Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ametunukiwa Tuzo ya Uongozi Bora kutoka kwa Taasisi isiyo ya Serikali ijulikanayo kama NITETEE Foundation inayojihusisha na utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazoikabili Jamii katika kutambua mchango wake kama Kiongozi Kioo Mwanamke anayesaidia Jamii bila kujali tofauti zao ikiwa ni muendelezo wa Maadhimisho ya Sherehe za Siku ya Mwanamke Duniani iliyofanyika Mwanza Hotel na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mkuu wa Wilaya Ilemela na Madiwani Wanawake wa Manispaa hiyo

Akitoa Tuzo hiyo kwa Mhe Dkt Mabula Kiongozi wa Taasisi ya NITETEE Ndugu Frola Lauo amesema
'... Tumeamua kumpa Tuzo Dkt Angeline Mabula ikiwa ni Ishara ya kuutambua mchango wake kama Kiongozi Kioo Mwanamke ktk kusaidia Jamii bila kujali tofauti walizonazo. ..' 

Mbali na hayo Lauo ameongeza kuwa Mhe Mabula amekuwa msaada mkubwa kwa wakina Mama wasiojiweza sambamba na kuwataka Viongozi wengine hasa Wanawake kuiga mfano wake
Kwa upande wake Mhe Mabula ameishukuru Taasisi ya NITETEE kwa kuuona mchango wake ktk Jamii na kuwahakikishia kuwa ataendelea na Jitihada za kuhakikisha anawasaidia Wanawake sanjari na kushirikiana na Taasisi zote zisizo za Serikali kumsaidia Mwanamke huku akiwataka Wanawake wote nchini kushirikiana ktk kuzifikia ndoto zao

'...  Wewe pale ulipo kama Mama ni lazima ujiulize nini umefanya Wanawake wengine waweze kuiga kutoka kwako, Umefika wakati sasa wakufungua milango wengine waweze kuingia ndani ulipo na ni lazima tuwezeshane ili kulifikia jukumu kubwa la kuifikia Tanzania ya viwanda na Sisi wakina Mama ndio tuliopewa jukumu hili kama kauli Mbiu ya Siku ya Mwanamke inavyoeleza. ..'

Mbali na Dkt Mabula wanawake wengine waliopewa Tuzo mbalimbali ni Mhe Maria Nyerere, Mhe Getrude Mongela, Mhe Anna Tibaijuka,  Mhe Vicky Kamata na Taasisi ya The Angeline Foundation

Imetolewa na

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
09.03.2017


0 comments:

Post a Comment