Wednesday, April 5, 2017

UGENI WA WAWEKEZAJI KUTOKA NCHINI KOREA WAWASILI RASMI NCHINI





Ile ndoto ya kuifikia Ilemela yenye neema ya mafanikio inaelekea kutimia kufuatia kuwasili kwa ugeni wa wawekezaji kutoka nchini Korea Kusini uliowasili mapema nchini kwa kuanza utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya Manispaa ya Ilemela .

Ikumbukwe kuwa kuwasili kwa ugeni huu kunakuja kufuatia ziara aliyoifanya Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi mapema  mwaka Jana na baadae Viongozi wa Manispaa Ilemela wakiongozwa na Meya wa Manispaa hiyo Mheshimiwa Renatus Mulunga akiambatana na Mkurugenzi wake John Wanga kwa kuitembelea miji rafiki ya nchini Korea kwa lengo la kubadilishana uzoefu, kuingiwa kwa mikataba mbalimbali ya shughuli za maendeleo na Uwekezaji.

Kabla ya kuwasili wilayani Ilemela hapo siku ya alhamisi kwa utekelezaji wa shughuli za kimaendeleo  Ugeni huu wa Uwekezaji hapo kesho siku ya jumatano unataraji kukutana na Viongozi wa Wizara ya fedha, Wizara ya Majii na Umwagiliaji na baadae Wizara ya Afya

  '... Ilemela ni yetu,Tushirikiane kuijenga ...' 


Imetolewa na  
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
04.04.2017

KAMATI MAALUMU YA JESHI LA WANANCHI YA KUBAINI MIPAKA YAANZA KAZI





Kamati maalumu ya Jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ kutoka makao makuu ikiongozwa na mkuu wa kikosi cha Anga 601 Meja BM Msilu imeanza kazi rasmi leo ya kubaini upya mipaka ya jeshi hilo ili kumaliza sintofahamu ya kimipaka baina ya jeshi hilo na wananchi wa maeneo jirani.

Mbali na Jeshi kamati imejumuisha viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Katibu wa ofisi ya Mbunge Jimbo la Ilemela, Kaimu Katibu Tawala wa wilaya Ilemela, Afisa Ardhi Kanda ya Ziwa na Wapima Ardhi kutoka Halmashauri ya Manispaa Ilemela.

Aidha kuanza Kazi kwa kamati hii ni utekelezaji wa ahadi ya Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Dkt Angeline Mabula aliyoitoa  mapema mwanzoni mwa mwaka huu alipokuwa akizungumza na wananchi wa maeneo yanayokabiliwa na migogoro ya mipaka na kuahidi kuyashughulikia haraka iwezekanavyo ili kutoa fursa kwa wananchi wa maeneo hayo waweze  kuendelea na shughuli za kujiletea maendeleo sanjari na kuepusha changamoto zinazoweza kuchochewa na migogoro hiyo .

Akizungumza katika zoezi hilo Afisa wa Ardhi kutoka Kanda ya Ziwa Bwana Eliah Kamihanda amesema
‘… Kazi yetu kubwa ni kubaini uhalisia wa mipaka ya Jeshi na wananchi ili baada ya Zoezi kutoa fursa ya maamuzi yenye haki na usawa kwa pande zote mbili kwa lengo kusaidia utatuzi wa migogoro ya mipaka …’ 

Nae Katibu wa Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Ilemela Ndugu Kheri James amesema kuwa  lengo la Mhe Mbunge pamoja na Uongoz wa wilaya ni kuona migogoro yote ya Ardhi ndani ya Jimbo kati ya Wananchi na Taasisi au Wananchi na Wananchi inakwisha,  

Hivyo hizi ni sehemu ya Juhudi  za Mhe Mbunge kwa kushirikiana na Mamlaka nyengne kuona migogoro hiyo inakwisha, Tunawasihi wananchi kutoa ushirikiano kwa kamati inapopita katika maeneo yao sambamba na kujiepusha na manunuzi au matumizi ya ardhi bila kufuata taratibu 


Imetolewa na 
Ofisi ya Mbunge 
Jimbo la Ilemela
04. 04. 2017

Thursday, March 9, 2017

MBUNGE WA JIMBO LA ILEMELA ATUNUKIWA TUZO YA UONGOZI BORA






Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ametunukiwa Tuzo ya Uongozi Bora kutoka kwa Taasisi isiyo ya Serikali ijulikanayo kama NITETEE Foundation inayojihusisha na utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazoikabili Jamii katika kutambua mchango wake kama Kiongozi Kioo Mwanamke anayesaidia Jamii bila kujali tofauti zao ikiwa ni muendelezo wa Maadhimisho ya Sherehe za Siku ya Mwanamke Duniani iliyofanyika Mwanza Hotel na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mkuu wa Wilaya Ilemela na Madiwani Wanawake wa Manispaa hiyo

Akitoa Tuzo hiyo kwa Mhe Dkt Mabula Kiongozi wa Taasisi ya NITETEE Ndugu Frola Lauo amesema
'... Tumeamua kumpa Tuzo Dkt Angeline Mabula ikiwa ni Ishara ya kuutambua mchango wake kama Kiongozi Kioo Mwanamke ktk kusaidia Jamii bila kujali tofauti walizonazo. ..' 

Mbali na hayo Lauo ameongeza kuwa Mhe Mabula amekuwa msaada mkubwa kwa wakina Mama wasiojiweza sambamba na kuwataka Viongozi wengine hasa Wanawake kuiga mfano wake
Kwa upande wake Mhe Mabula ameishukuru Taasisi ya NITETEE kwa kuuona mchango wake ktk Jamii na kuwahakikishia kuwa ataendelea na Jitihada za kuhakikisha anawasaidia Wanawake sanjari na kushirikiana na Taasisi zote zisizo za Serikali kumsaidia Mwanamke huku akiwataka Wanawake wote nchini kushirikiana ktk kuzifikia ndoto zao

'...  Wewe pale ulipo kama Mama ni lazima ujiulize nini umefanya Wanawake wengine waweze kuiga kutoka kwako, Umefika wakati sasa wakufungua milango wengine waweze kuingia ndani ulipo na ni lazima tuwezeshane ili kulifikia jukumu kubwa la kuifikia Tanzania ya viwanda na Sisi wakina Mama ndio tuliopewa jukumu hili kama kauli Mbiu ya Siku ya Mwanamke inavyoeleza. ..'

Mbali na Dkt Mabula wanawake wengine waliopewa Tuzo mbalimbali ni Mhe Maria Nyerere, Mhe Getrude Mongela, Mhe Anna Tibaijuka,  Mhe Vicky Kamata na Taasisi ya The Angeline Foundation

Imetolewa na

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
09.03.2017


Wednesday, March 8, 2017

WAWAKILISHI WA WANANCHI WATAKIWA KUYASIMAMIA MASLAHI YA WANAWAKE






Wawakilishi wa wananchi kwa ngazi mbalimbali za Uongozi wametakiwa kuyasimamia na kuyaweka mbele maslahi ya wanawake wanapokuwa katika vikao vyao vya maamuzi     

Hayo yamebainishwa leo na Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alipokuwa akizungumza na Wanawake wa Mkoa wa Mwanza katika kilele cha maadhimisho ya sherehe za siku ya Wanawake Duniani yakiwa na Kauli Mbiu kuwa Tanzania ya Viwanda 

Wanawake ni Msingi wa Mabadiliko Kiuchumi ambapo kimkoa yamefanyika Viwanja vya Furahisha wilayani Ilemela yakitanguliwa na Maandamano ya amani kutoa Viwanja vya Shule ya Sekondari Baptist

Akizungumza katika maadhimisho hayo MheshimiwaDkt Mabula amesema kuwa umefika wakati kwa viongozi wa ngazi mbalimbali kuweka maslahi ya Wanawake mbele na kuyasimamia ili kulikwamua na kulisaidia kundi hili kubwa linalonyanyaswa na kuonewa katika Nyanja mbalimbali za kimaendeleo

Aidha amewasisitiza Viongozi wanawake waliopata fursa kuwa mbele katika kuhakikisha wanasaidia wanawake wenzao na watoto ili kuzifikia ndoto zao

‘… Niwatake viongozi wenzangu mnapokaa katika vikao vya maamuzi jicho lako la kwanza litazame nini kimetengwa kwa maslahi ya wanawake wa eneo lako, Tega masikio ni kipi kipo kule na Sisi tuliopewa nafasi lazima tuoneshe kuwa tunaweza kwa kuweka wanawake wenzetu mbele …’

Aidha amewataka wanawake kuwekeza katika fursa tofauti tofauti za kiuchumi zinazojitokeza ikiwemo ununuzi wa hisa za makampuni nchini

Nae Marry Mhoha akisoma risala kwa niaba ya wengine ametaka kupewa kipaumbele kwa wanawake katika nafasi za Uongozi kuhakikisha wanayatatua matatizo yao kupitia nafasi hizo

Akihitimisha Sherehe hizo Mbunge wa Viti Maalum kupitia Mkoa Mwanza Mheshimiwa Kiteto Zawadi Koshuma amemshukuru Daktari Mabula kwa kujumuika pamoja nao na kumhakikishia kuwa wanatambua mchango wake ktk kuwatumikia wanawake na jamii kwa ujumla


Imetolewa na

Ofisi ya Mbunge 
Jimbo la Ilemela
08.03.2017

Sunday, February 26, 2017

MBUNGE WA JIMBO LA ILEMELA AMJULIA HALI MSANII JET MAN.











Katika hali ya kukutana na makundi na watu mbalimbali ndani ya jimbo,Mh Mbunge wa jimbo la Ilemela Dkt.Angeline.S.L.Mabula amemtembelea  nyumbani kwao msanii Jet Man ambae ameugua kwa takribani miaka mitano bila kuamka kitandani kutokana na tatizo la kupooza sehemu ya mwili.

Akiwa nyumbani hapo mh.Mbunge amempa pole msanii huyo na kuahidi kushirikiana na watu wengine waliojitolea ktk jamii kusaidia matibabu ya msanii huyo.Mh.Mbunge amesaidia vifaa na mahitaji mbalimbali ili kumsaidia japo kwa uchache ndugu yetu huyo.Jet Man ni miongoni mwa vijana wa Ilemela walio vuma saana ktk mziki wa kizazi kipya ktk siku za nyuma.

Niimani yetu kila mmoja wetu akiguswa na tunaweza kumsaidia Jet Man kurejea ktk afya yake.
                       
"Ilemela ni yetu,tushirikiane kuijenga".  

                       
Imetolewa na.               
Ofisi ya mbunge.         
Jimbo la Ilemela-Mwanza

Thursday, February 23, 2017

WIZARA YA ARIDHI NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI,YAHAMIA RASMI MJINI DODOM.






Mbunge wa jimbo la Ilemela na naibu Waziri wa Aridhi Dkt.Angeline S.L.Mabula ajumuika na watumishi wenzake wa wizara ya aridhi ktk zoezi la kupaki vifaa na vitendea kazi tayari kwa safari ya kuhamia rasmi mjini Dodoma.Hatua hii ni utekelezaji wa agizo la Mh.Rais Dkt.John Pombe Magufuri lakuitaka serikali kuhamia makao makuu ya nchi mjini.


Wizara mbalimbali tayari zimehamia mjini humo zikiongozwa na mh.Waziri mkuu mh.Kassim Majaliwa ambae alikuwa wakwanza kuongoza zoezi hilo.

Friday, February 17, 2017

MAKAMU WA RAIS MHE SAMIA AZURU ILEMELA















Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ndo Mlezi wa Halmashauri ya Manispaa Ilemela Mheshimiwa Samia Suluhu amefanya Ziara Ilemela ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa mapema mwishoni mwa mwaka jana wakati wa ufunguzi rasmi wa Jengo la Halmashauri ya Manispaa hiyo

Akizungumza katika mkutano uliojumuisha Viongozi mbalimbali wa ngazi za mitaa, kata, wilaya, Mkoa na watumishi wa Manispaa hiyo Mheshimiwa Samia mbali na kutoa Pongezi kwa jitihada za kimaendeleo zinazofanywa ameitaka Ilemela kuanzisha mikakati katika kupambana na vita ya madawa ya kulevya , uvuvi haramu sambamba na uanzishwaji wa jukwaa la wanawake lenye lengo la kumwezesha mwanamke kujikwamua kiuchumi na kutatua changamoto zinazowakabili

'... Niliahidi nikikanyaga Mwanza ni lazima nifike Ilemela na hii ni kwasababu Ilemela mpo teyari kwa kazi inayojidhihirisha kwa mafanikio mliyoyapata hasa kwenye sekta ya Elimu...'
Akimkaribisha  Makamu wa Rais Mkuu wa Mkoa Mwanza Mheshimiwa John Mongela amemuhakikishia kuwa anaridhishwa na kasi ya maendeleo inayofanywa na Ilemela sambamba na hatua nzuri katika ukusanyaji wa mapato

'... Ilemela ni miongoni mwa Halmashauri tegemezi kwa Mkoa wetu katika ukusanyaji wa mapato hivyo niwapongeze sana Madiwani, Mkurugenzi na watendaji wote kwa utendaji kazi wao katika kuleta mabadiliko...'
Akisoma taarifa yake Mkurugenzi wa Ilemela John Wanga kwa niaba ya Mkuu wa wilaya hiyo Daktari Leonard Masale mbali na utekelezaji wa Maagizo ya Mheshimiwa Makamu wa Rais aliyoyatoa katika Ziara yake ya awali amemuomba kuisaidia Manispaa hiyo juu ya umaliziaji wa miradi yake ya maji, barabara, ulipaji wa fidia za ardhi na hospitali jambo ambalo Mlezi huyo aliahidi kulifanyi kazi

Akihitimisha Mbunge wa Jimbo hilo na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Daktari Angeline Mabula amemshukuru Mheshimiwa Makamu wa Rais kwa Uamuzi wake wa kuzuru Ilemela na kumsisitiza kutomchoka kwa kipindi chote atakachokuwa akimsumbua katika kuhakikisha wanaungana katika kuletea maendeleo ya Ilemela

'... Ilemela ni yetu, Tushirikiane kuijenga...'


Imetolewa na
Ofisi ys Mbunge
Jimbo la Ilemela
16.02.2017